Habari Na, Khadija Nassor
Picha kutoka maktaba
Mwenyekiti wa kamati ya skuli ya msingi Konde A Khamis Juma Khamis amesema, Ushiriki nzuri wa viongozi wanawake kwenye ngzi ya jamii ni nyenzo muhimu katika harakati za kuleta maendeleo nchini.
Ameyasema hayo mara baada ya mwandishi wa habari hizi kufika skulini hapo.
Aidha ameongeza kua kampeni ya elimu iliyofanywa na kiongozi Zawadi imekua mkombozi kwao na wanafunzi kwa ujumla ,kwani imewaongezea ufanisi katika utendaji wa majukumu yao sambamba na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu skuli ya Konde A msingi Abdi Omar Ali sambamba na walimu wanaofundisha masomo tofauti, Salma Mohd na Zafaran Said Abdalla wamesema wamepata mabadiliko makubwa tangu kuanza kwa kampeni hiyo uklilinganisha na hapo awali.
Nae mwakilishi wa Jimbo la Konde Zawadi Amour Nassor amesema kilichomsukuma kuanzisha kampeni hiyo ni kuona urithi nzuri kwa vijana ni elimu hali itakayosaidia kuongeza idadi ya ushiriki kwenye ngazi tofauti ndani ya jamii na serikali kwa ujumla.
Akitaja chanzo cha fedha alichoendeshea kampeni hiyo amesema ni juhudi zake binafsi sambamba na kuongeza wigo wa mashirikino kutoka kwa viongozi wenzake wa majimbo jirani.
Taarifa kutoka skuli ya msingi Konde A yenye jumla ya wanafunzi 1783 zimeonesha mwaka 2020 jumla ya wanafunzi 122 wa darasa la 6 wamesajiliwa , 117 walifanya mtihani na 17 wamepasi michipuo, , huku 2021 jumla ya wanafunzi 228 wamesajiliwa, wote wakafanya mtihani na 25 wakapasi michepuo na 1 akapasi kipawa hali iliyopelekea kushika nafasi ya 4 kiwilaya na mwaka jirani wa 2022,jumla ya wanafunzi 100 wamesajiliwa , 98 wakafanya mtihani na kutoka michepuo wanafunzi 12.
[4/21, 07:45] Khadija Nassor: Mwenyekiti UV CCNM Wete awanoa vijana.
Vijana wa UVCCM Wilaya ya Wete wamesema juhudi zinazochukuliwa na mwenyekiti wao Sada Saleh zimesaidia vijana hususani wanawake kujitambua na kushiriki kwenye Demokrasia Siasa na Uongozi.
Wakizungumza nami mara baada ya kufika ofisi kuu ya CCM Wilayani Wete Zainab Mkubwa Mohd, Khairat Ali Juma na Hemed Juma Salum miongoni mwa waliopata mafunzo ya itikadi na uongozi wamesema mafunzo hayo yamewakomboa kama vijana na kuahidi kuendelea kufanyia kazi ili kupanua wigo wa kimaendeleo.
Akijibu suali la ni kwa namna gani ameendesha mafunzo hayo kwa vijana Mwenyekiti Sada amesema.
Ni kutokana na juhudi zake sambamba na usaidizi wa mbunge wa jimbo la Kojani ambapo zilikua chachu ya kukamilisha ndoto zake kwa vijana.
Nae Nassor Hakim Haji, msaidizi wa sheria Wilaya ya Mkoani amefafanua kwa kusema, Wanawake wana uweo sawa kama wanaume hivyo ni vyema kuaminiwa na kupewa nafasi za kuongoza kwani ni haki yao kidemokrasia.
Jumla ya vijana 135 kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA tawi la Pemba samba na viongozi tofauti wa chama cha CCM Wilaya ya Wete wamepatiwa mafunzo ya uongozi ambapo 85 ni wanawake.
Khadija Nassor: Mwenyekiti wa umoja wa wanawakke Tanzania, UWT Taifa ,kupitia Chama Cha Mapinduzi Mary Chatanda , amewataka wananchi kuthamini na kutunza juhudi za mbunge Maida anazozionesha kwao ili lengo lengo la kuwanyanyua wanawake Mkoa wa Kaskazini Pemba lifikiwe kiufanisi.
"Napongeza juhudi za kimaendeleo zinazofanywa na mbunge Maida Hamad Abdallah ni mfano wa kuigwa kwa viongozi, Hivyo hamuna budi na nyinyi jamii kuthamini na kutunza ili kufikia lengo na kujikomboa kimaisha". Amesema mwenyekiti.
Aidha mwenyekiti amekupokea mashuka na delivery kit” kwa ajili ya wodi ya mama na mtoto kwa ajili ya Hospitali ya Micheweni vyenye thamani ya Tzsh milioni 1 na laki 1 (1,100,000) sambamba na mchelele polo 4 za kilo hamsini, unga wa sembe kilo 25,maharage kilo 25kwa ajili ya watoto wanaojiandaa na mitihani ya darasa la nne, saba , kidato cha pili na cha nne zenye gharama ya tsh 556,00/=
Nae Makamu mwenyekiti wa umoja huo Zainab Shomari amepongeza hatua ya kiongozi maida mkoani humo.
Akabidhiwa sare za pili kwa wanafunzi yatima 20 wanaosomeshwa kupitia msaada wa mbunge huyo katika skuli ya Lurent English Medium iliopo Ole Kianga , ambao watasoma kuanzia maandalizi, msingi, sekondari kwa thamani ya tsh miliioni 35 kila mwaka hiyo ikijumuisha ada usafiri, sare za pili pamoja na zawadi nyengine ikiwemo vinywaji, chakula na sukari kwa ajili ya kupikiwa uji wanafunzi wa maandalizi.
Kwa upande wao walimu na wanafunzi wa skuli ya Laurent wameshukuru kwa msaada waliopatiwa kwani baadhi ya wanafunzi hao mbali ya kua ni mayatima ila wanatoka kwenye mazingira magumu, yanayopelekea kukosa muda wa kujisomea.
"Tunajisikia vizuri kama walimu kwa juhudi anazozifanya bi Maida kwa kuona umuhimu wakusaidia kundi hili kwani awali walipoletwa hapa na sasa ni tofauti" amesema mwalimu Khamis Marshed.
"ninajisikia faraja kupata nafasi hii kwani imenifanya niweze kusoma kwa juhudi na kufanya vizuri kwenye mitihani, awali ilikua natokea wa mbali sana darasani ila kwa sasa nashika nafasi ya tatu, ya pili nay a kwanza." amesema mwanafunzi Ahmed Omar
Jumla ya watoto yatima 180 wanasoma skuli ya lauent English medium kupitia juhudi za mbunge huyo na Jumuiya yake ya UMAWEZA ambapo yeye ni Mwenyekiti yenye lengo la kuboresha masomo ya Sayansi kwa Wanawake Zanzibar.
Khadija Nassor: Wanawake kisiwani pemba wamezitaka taasisi binafsi na zile za serikali kuandaa mazingira rafiki itakayowawezesha kuripoti vitendo vya rushwa pindi wanapotia nia za kushiriki kwenye ngazi za maamuzi.
Ameyasema hayo Asha Said kutoka chama cha CUF na Halima Mohamme Babu kutoka CCM wakizungumza na mwandishi wa habari hizi na kuongeza kua wanawake wanakosa ujasiri wa kushitaki matendo hayo kwa kuhofia usalama wao.
Mohammed Najim kutoka mwevuli wa asasi za kiraiya Pemba PACSO amesema wamekua wakitoa elimu juu ya kuripoti kwa kadhia hizo na kuwataka wanawake kujitokeza kutumia haki yao ya kidemokrasia.
Kwa upande wake afisa kutoka Mamlaka ya kuzuiya rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar afisi ya Pemba Kassim Yussuf Ali amewatoa hofu wanawake na kuahidi kutembea hadi vijijini kutoa elimu ya uripoti rushwa kwa jamii hususan wanawake kua huru kwenye harakati zao.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ibara ya 21 ibara ndogo ya 1 imetoa haki kwa kila Mzanzibari kushiriki katka shughuli za utawala wa nchi ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa kwa hiari.
ReplyForward |
Comments
Post a Comment