Skip to main content

Mkurugenzi TAMWA ZNZ awashukuru wadau kufanikisha zoezi la utoaji tuzo kwa waandishi wa habari 2024.

MKURUGENZI Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, TAMWA ZNZ kwa niaba ya ZAFELA na PEGAO ametoa shukrani za dhati kwa wote waliochangia kufanikisha hafla ya utoaji tuzo kwa waandishi wa habari iliyofanyika Jumamosi, Machi 9, 2024, katika Ukumbi wa SHAA mjini Unguja.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko ofisi za TAMWA ZNZ Tunguu, Mkurugenzi wa TAMWA ZNZ, Dkt. Mzuri Issa ametoa pongezi kwa waandishi wote waliowasilisha kazi zao kwa ajili ya kushiriki tunzo za umahiri wa waandishi wa habari za wanawake na uongozi.

Tuzo hizo zilitolewa katika vipengele vinne tofauti ikiwemo Radio Jamii, Radio za kitaifa, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo habari zilizowasilishwa zilikua zikiangazia maeneo mbalimbali ya kupigania haki za wanawake na mabadiliko.

Washindi wa tuzo hizo walizawadiwa zawadi ya vyeti, ngao pamoja na fedha taslim ambapo mshindi wa jumla ni Amina Masoud aliyezawadiwa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tatu za Kitanzania, ikionesha kutambuliwa kwa mchango wake wa kipekee katika tasnia hiyo.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Jaji Mkuu wa Tuzo hizo Dkt. Abdalla Mohammed Juma alisema waandishi wa habari wanawake wameonesha muamko mkubwa katika kuwasilisha kazi zao ambapo katika waandishi wote walioleta kazi wanawake walikua ni 379.

Dkt. Abdalla aliongeza kuwa kazi hiyo ya kuwatafuta washindi wameifanya kwa uadilifu mkubwa kuhakikisha washindi waliopatikana ni wale waliowasilisha kazi zenye ubora.

“Kazi tuliyopewa tumeifanya kwa uadilifu mkubwa, na kama kuna mapungufu ni sisi majaji tunayabeba mapungufu hayo kwa asilimia 100”, Dr. Abdalla Mohammed alisema Jaji.

Bi Nasra Mohammed, mwandishi wa habari mkongwe ambae pia alikua ni miongni mwa majaji amewahimiza waandishi kuandika kazi zao katika viwango vya juu ili kuweza kuisaidia jamii katika masuala hayo ya takwimu.

"Sisi waandishi wa habari tufanye kazi kwa bora na zenye viwango kila siku ili kuweza kuipasha jamii taarifa sahihi zilizoshiba na kuleta tija katika jamii." Alisema Bi Nasra

Mwisho Dkt Mzuri alitoa wito kwa waandishi wa habari kuendelea kuandika habari zinazohusiana na wanawake, ikiwa ni pamoja na changamoto zinazokwamisha upatikanaji wa nafasi za uongozi.

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kufanyika kwa tuzo hizi, na kwa mwaka huu kumekua na ongezeko kubwa la idadi ya kazi zilizowasilishwa ambapo jumla ya kazi 529 kutoka vyombo vya habari mbalimbali Zanzibar ziliwasilishwa.

Tuzo hizi zinafanyika ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi ambao unatekelezwa na TAMWA ZNZ, ZAFELA na PEGAO kwa ushirikiano mkubwa na ubalozi wa Norway ambapo Kaulimbiu ya Tuzo hizi ni "Kalamu Yangu, Mchango Wangu kwa Wanawake" inayoakisi dhamira endelevu ya waandishi wa habari kuongeza sauti za wanawake na kuchangia katika maendeleo yao.


Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...