Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2025

JUHUDI ZA WAANDISHI NA WADAU WA SHERIA ZA HABARI ZANZIBAR, ZAZAA MATUNDA-TAMWA,ZNZ.

NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA  Jumla ya makala 253, zinazohusu masuala ya uhuru wa habari Zanzibar zimeripotiwa na kuchapishwa kupitia magazeti, redio za kijamii na kitaifa pamoja na mitandao ya kijamii. Makala hizo zimeandikwa na waandishi wa habari 25 waliopata mafunzo maalum kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya Unguja na Pemba. Hayo yameelezwa na Afisa Programu ya Mapitio ya sheria na uhuru wa habari kutoka TAMWA-ZNZ, Zaina Abdalla Mzee, wakati akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa programu hiyo. Katika wasilisho hilo Zaina alibainisha mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza pamoja na mikakati ya baadaye kwa ajili ya kuendeleza juhudi za kulinda na kuimarisha uhuru wa habari visiwani Zanzibar. Zaina alibainisha kuwa juhudi za ushawishi na uchechemuzi zilizofanywa na wadau wa habari, wakiwemo Wajumbe wa Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO), waandishi na wahariri habari, zimezaa matunda kwa kufanikisha kufanyika kwa mikutano mbalimbali na baadhi ya...

VYAMA VYA SIASA VYAPEWA KIBARUA, KUWATEUA WANAWAKE UCHAGUZI MKUU 2025.

Wadau wa masuala ya wanawake na uongozi wamevitaka vyama vya siasa nchini kuhakikisha vinawateua wanawake waliokidhi vigezo kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, hususan kwenye nafasi za uwakilishi, ubunge na udiwani zinazoshindaniwa majimboni. Wakizungumza katika taarifa yao kwa vyombo vya habari, wadau hao wameeleza kuwa kwa muda mrefu wanawake wamekuwa wakipewa nafasi za viti maalum pekee, hatua inayowanyima nafasi ya kushindana moja kwa moja na wanaume na kuonesha uwezo wao katika siasa za ushindani. Katika kipindi hiki cha mchakato wa chaguzi za ndani ya vyama kuelekea uchaguzi mkuu, wanawake wengi wamejitokeza kuchukua fomu, licha ya kuwa idadi yao bado ni ndogo kulinganisha na wanaume. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu Zanzibar, wanachama 1,640 wamechukua na kurejesha fomu za kugombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani, ambapo kati yao wanawake ni 406, sawa na asilimia 24.7. Chama cha ACT Wazalendo kwa upande wake kimerip...

Upatikanaji wa Sheria Mpya ya Habari Zanzibar, bado Kitendawili.

 NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Afisa programu ya mapitio ya Sheria za Habari na Uhuru wa Habari na kujieleza kutoka Tamwa, Zanzibar Zaina Abdalla Mzee, amesema licha ya Wanaharakati, wadau na waandishi wa Habari Visiwani Zanzibar kupaza sauti juu ya kufanyiwa marekebisho Sheria za Habari suala ambalo bado halijafanyiwa kazi ipaswavyo ingawa Baraza la Wawakilishi limeahidi kulifanyia kazi suala hilo katika msimu ujao wa vikao vya Baraza hilo. Akiwasilisha ripoti kwa Waandishi wa Habari katika Ofisi za Tamwa Mkanjuni Pemba jana Tarehe 24\07\2025, ripoti yenye lengo la kuonesha hali halisi iliyofikiwa kwa kipindi cha miaka miwili ya utekelezaji wa mradi wa miaka miwili unaofadhiliwa na Shirika la #CommonWealth, ripoti iliyoonesha kuwepo kwa Sheria kandamizi kwa vyombo vya Habari, wanahabari na uhuru wa kujieleza kwa wananchi Visiwani Zanzibar. "Miongoni mwa matokeo (Outcomes) ya mradi huu ni pamoja na kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari kuzitambua Sheria za Habari kuona mapungufu yali...

WANAWAKE WAHIMIZWA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KUTANGAZA KAZI ZAO

 NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Meneja miradi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) Nairat Abdulla amewaomba wanawake kutumia vyombo vya habari kwa lengo la kutangaza kazi zao wanazozifanya. Akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wakulima viongozi kutoka shehia nne (4) za Unguja, juu ya umuhimu wa kutumia vyombo vya habari, yaliofanyika ofisi za TAMWA-ZNZ Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja, amesema wanawake wanajishughulisha na harakati mbalimbali zikiwemo za uzalishaji pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi lakini bado sauti zao hazisikiki ipasavyo kupitia vyombo vya habari. Hivyo amewaomba wanawake hao kutumia vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii, kuelezea mafanikio na changamoto zinazowakabili katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili kufikisha ujumbe kwa wahusika na hatimae kupatiwa ufumbuzi. Akiwasilisha mad a inayohusu vyombo vya habari, Meneja Mawasiliano kutoka TAMWA ZNZ, Sofia Ngalapi amesema wanawake wakulima...