Zanzibar hakuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, tumeani elimu kidogo kuhusu Chaguzi.
Hivi karibuni huko Tanzania Bara kumekuwa na mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo leo Novemba 27, 2024 Wananchi wanapiga kura.
Mimi kama mdau wa siasa na mifumo ya Uchaguzi Zanzibar nimekuwa nikipokea maswali mengi kuhusu kwanini Zanzibar kumekuwa hamna shamrashamra za Uchaguzi kama ilivyo Bara.
Nianze kwa kusema kuwa huku Visiwani, kwa miaka yote hakuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Viongozi wote wa Serikali za Mitaa huteuliwa na viongozi wa Serikali Kuu hawachaguliwi na wananchi kama ilivyo Tanzania bara kwa nafasi hiyo.
Huku Zanzibar kwa ngazi ya chini kabisa ya Serikali za Mitaa huwa tuna Masheha ambao kwa Bara ni kama viongozi wa Kata.
Hawa Masheha huteuliwa na Wakuu wa Mikoa na huwa wako kwenye level ya chini kabisa ya Uongozi.
Ukitoa ngazi ya Sheha anayefuata ni mtu wa Halmashauri alafu ndo anakuja Mkuu wa Wilaya ambao wote wawili yaani mtu wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya wanateuliwa na Rais.
Kwa ujumla sisi wananchi wa Zanzibar hatuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Badala yake huwa tunashiriki kwenye Uchaguzi Mkuu ambapo katika Uchaguzi Mkuu sisi huchagua viongozi watano ambao ni Diwani, Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi, tunapiga na Rais wa Zanzibar alafu tunapiga na zile mbili za Bara ambazo ni za Mbunge pamoja na Rais.
Comments
Post a Comment