Posts

Showing posts from March, 2024

AJALI YAUA WAANDISHI WA HABARI WAWILI WA MKOA WA LINDI.

Image
WATU wawili ambao ni waandishi wa habari mkoa wa Lindi wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali . Ajali hiyo iliyohusisha gari dogo imetokea majira ya usiku wa kuamkia Leo March 26 eneo la Nyamwage mkoani mkoa wa kipolisi Rufiji (Pwani) Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo Alli Husein alisema Waandishi hao walikuwa wanatokea Dar es Saalam kwenye mafunzo kurejea mkoani Lindi . Waandishi waliofariki dunia ni Abdalla Nanda wa Chanel Ten mkoa wa Lindi na Josephine Kibiriti wa Sahara Media Group. M atukio Daima media kumtafuta kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Rufiji (Pwani)Protasi Mutayoka amethibitisha kutokea Kwa Ajali na kuwa Ajali hiyo ilitokea majira ya Saa 7 usiku wa March 26 na Chanzo ni Dereva wa Centar ambae baada ya ajali alikimbia na msako wa kumtafuta unaendelea. Alisema kuwa kwenye gari ndogo ya waandishi walikuwa watu watatu na Wawili Mwanamke mmoja na mwanaume walifariki Dunia eneo la tukio na mmoja ni majeruhi amelazwa Hospitali na mguu ...

Weledi, umahiri katika kada ya habari ni nguzo muhimu.

Image
Waandishi wa habari wametakiwa kufuata kwa kina maadili ya waandishi wa habari ili kukuza weledi na umahiri wa kada ya habari na kuzifanya taasisi za kihabari ziweze kuaminika na kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Akizungumza na wadau wa habari katika ziara yake iliyofanyika Zanzibar tarehe 23 na 24 Machi katibu mtendaji wa baraza la habari Tanzania Ernest Sungura amesema kuwa  katika kufuata maadili hayo pia suala la kuzingatia vyanzo anuai vya habari havina budi kupewa kipaumbele. “Mara nyingi waandishi wetu wamekuwa na maradhi ya chanzo kimoja cha habari hali hii inapaswa kubadilika ili habari zetu ziweze kuwa na mawanda mapana zaidi na vyanzo vingi na tofauti vya habari”, alisisitiza. Amesema kuwa nguvu ya vyombo vya habari haina budi kutumika katika kujenga jamii iliyo bora na hivyo sauti za watu hazina budi kupewa kipaumbele. “taasisi za habari na vyombo vya habari havina budi kubadilika ili sauti za makundi ya pembezoni ikiwemo wanawake na vijana ziweze kusikika tuwape s...

Mradi wa "SWIL" wawezesha akina Mama zaidi ya 50 kujua kusoma na kuandika Shehia ya Mjini Kiuyu.

Image
Imeandikwa na Hassan Msellem, Pemba  Mradi wa Uhamasishaji wanawake kushiriki katika Uongozi (SWIL) unaoendeshwa na taasisi tatu ambazo ni Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar, Jumuiya Utetezi wa Mazingira na Kijinsia Pemba (PEGAO) pamoja na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) kupitia madarasa ya kisomo Shehia ya Mjini Kiuyu umefanikiwa kuongeza idadi ya akina mama wenye uwezo wa kujua kusoma na kuandika ili waweze kushiriki vyema katika shughuli za kijamii, kisiasa na uongozi. Mariam Juma Hamad ni Mwalimu wa darasa la Kisomo Shehia ya Mjini Kiuyu amesema licha ya changamoto mbali mbali zinazolikabili darasa hilo lakini limeweza kutoa mwanga kwa akina mama wengi kujua kusoma na kuandika ikilinganishwa na hapo awali kabla ya kuanzishwa kwa darasa hilo. “Kwakweli darasa hili limetusaidia sana akina mama wa Shehia ya Mjini Kiuyu wengi walikuwa hawajui kusoma wala kuandika hata majina yao lakini tangu kuanzishwa kwa darasa hili ta...

Mkurugenzi TAMWA ZNZ awashukuru wadau kufanikisha zoezi la utoaji tuzo kwa waandishi wa habari 2024.

Image
MKURUGENZI Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, TAMWA ZNZ kwa niaba ya ZAFELA na PEGAO ametoa shukrani za dhati kwa wote waliochangia kufanikisha hafla ya utoaji tuzo kwa waandishi wa habari iliyofanyika Jumamosi, Machi 9, 2024, katika Ukumbi wa SHAA mjini Unguja. Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko ofisi za TAMWA ZNZ Tunguu, Mkurugenzi wa TAMWA ZNZ, Dkt. Mzuri Issa ametoa pongezi kwa waandishi wote waliowasilisha kazi zao kwa ajili ya kushiriki tunzo za umahiri wa waandishi wa habari za wanawake na uongozi. Tuzo hizo zilitolewa katika vipengele vinne tofauti ikiwemo Radio Jamii, Radio za kitaifa, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo habari zilizowasilishwa zilikua zikiangazia maeneo mbalimbali ya kupigania haki za wanawake na mabadiliko. Washindi wa tuzo hizo walizawadiwa zawadi ya vyeti, ngao pamoja na fedha taslim ambapo mshindi wa jumla ni Amina Masoud aliyezawadiwa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tatu za Kitanzania, i...

"Waandishi zidisheni juhudi kuandika juu ya Sheria kinzani dhidi ya uhuru wa Habari" Bi. Hawra.

Image
Imeandikwa na Hassan Msellem, Pemba. Waandishi wa Habari wametakiwa kuzidisha juhudi katika kuandika habari na makala kuhusu Sheria za habari zinazokinzana na Uhuru wa vyombo Habari ili ziweze kufanyiwa maboresho. Hayo yamesemwa na Mwandishi Mkongwe Visiwani Zanzibar Bi. Haula Shamte wakati akiwasilisha mada juu ya Sheria kinzani dhidi ya uhuru wa Habari katika Ofisi za Tamwa Kisiwani Pemba ambazo ni Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, magazeti na vitabu namba 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na Sheria namba 8 ya mwaka 2010, Sheria ya Tume ya Utangazaji namba 7 ya mwaka 1997 iliyofanyiwa marekebisho na Sheria namba 1 ya mwaka 2010. "Tukiangalia Sheria zote hizo tatu zinakinzana na falsafa ya Uhuru wa vyombo vya habari na Waandishi wa Habari kama ilivyoolezwa katika sura ya tatu ibara ya 18 ya katiba ya Zanzibar, hivyo basi ni jukumu letu wanahabari kuhakikisha tunaandika habari zaidi na makala mbali mbali Ili kuongeza ushawishi kwa vyombo vya kutunga Sheria katika kuzif...