MAKALA NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA. Ongezeko la madiwani wanawake katika ngazi mbali mbali Mkoa wa Kusini Pemba limekuwa ishara ya mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, pamoja na mwamko mpya wa jamii kutambua uwezo wa wanawake kama viongozi bora na chachu ya maendeleo. Miongoni mwa Madiwani Wanawake vijana waliopata fursa ya kuteuliwa kushika nafasi hizo na kuwawakilisha Wanawake wenzako vijana ni pamoja Amria Seif Saleh, ambaye ameteuliwa kuwa Diwani wa Baraza la Mji Mkoani na Fatma Khamis Ali, ambaye ni Diwani wa Wadi Kibokoni Vitongoji, wote wakiwa ni vijana chipukizi katika ulingo wa siasa na uongozi Kisiwani Pemba. Mabadiliko ya Kijamii na Kuongezeka kwa Uelewa k atika kipindi cha miaka ya karibuni, kumekuwa na kampeni mbalimbali zinazoendeshwa na mashirika ya kiraia, Serikali na taasisi binafsi zinazolenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi, Elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa usawa wa kijinsia na nafasi ya mwanamke katika maamuzi imechangia kwa kiasi kikubwa kupungu...