Posts

Showing posts from November, 2024

Zanzibar hakuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, tumeani elimu kidogo kuhusu Chaguzi.

Image
Hivi karibuni huko Tanzania Bara kumekuwa na mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo leo Novemba 27, 2024 Wananchi wanapiga kura. Mimi kama mdau wa siasa na mifumo ya Uchaguzi Zanzibar nimekuwa nikipokea maswali mengi kuhusu kwanini Zanzibar kumekuwa hamna shamrashamra za Uchaguzi kama ilivyo Bara.  Nianze kwa kusema kuwa huku Visiwani, kwa miaka yote hakuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.  Viongozi wote wa Serikali za Mitaa huteuliwa na viongozi wa Serikali Kuu hawachaguliwi na wananchi kama ilivyo Tanzania bara kwa nafasi hiyo. Huku Zanzibar kwa ngazi ya chini kabisa ya Serikali za Mitaa huwa tuna Masheha ambao kwa Bara ni kama viongozi wa Kata. Hawa Masheha huteuliwa na Wakuu wa Mikoa na huwa wako kwenye level ya chini kabisa ya Uongozi. Ukitoa ngazi ya Sheha anayefuata ni mtu wa Halmashauri alafu ndo anakuja Mkuu wa Wilaya ambao wote wawili yaani mtu wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya wanateuliwa na Rais.  Kwa ujumla sisi wananchi wa Zanzibar hatuna Uchaguzi wa ...

Salhida “ndoto yangu ni kuwa kiongozi na kuleta mabadiliko”

Image
Anzia nafasi ya Makamu wa rais Serikali ya wanafunzi Pindua Pemba    Wazazi wake, majirani, wamtaja mwenye kuona mbali  NA ZUHURA JUMA, PEMBA   SALHIDA Amour Rashid mwenye miaka 18, ni miongoni mwa vijana wa kike wenye ndoto za kufika mbali katika suala la uongozi. Kwa sasa yupo wa kidato cha nne katika skuli ya Sekondari ya Mohamed Juma Pindua wilaya ya Mkoani Pemba.  Akiwa skuli hapo kijana huyo, anaitumikia nafasi ya Makamu wa Rais katika serikali ya wanafunzi skulini hapo. "Ukiwa na malengo fulani katika maisha, ni lazima kutakuwa na vitu vingi vizuri, vikija utakuwa na hamu ya kuvifikia, lakini ikiwa sio kiongozi sio rahisi,’’anasema Salhida.  Skuli ya sekondari ya Mohamed Juma Pindua ina wanafunzi 969 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, huku serikali ya wanafunzi ikiwa na viongozi 14, wakiwemo wanawake wanne na wanaume 10.  Akiwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watano waliozaliwa katika kijiji cha Kidini Mkanyageni wilaya ya Mk...