Posts

Showing posts from September, 2024

“SMILE PEMBA MARATHON” KUBORESHA USTAWI WA WATU WENYE ULEMAVU

Image
  Na, Hassan Msellem- Pemba Wananchi Kisiwani Pemba wametakiwa kushiriki mashindano ya Mbio yanayobeba jina la Smile Pemba Marathon ili kufanikisha lengo la Mbio hiyo. Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Ahmed Abuubakar Mohammed huko Gombani Pemba, amesema lengp la Mbio hizo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kununua vifaa tiba na vifaa saidizi kwa watu Wenye Ulemavu. Aidha amesema Mbio hizo za hisani zinatarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2024, katika Uwanja wa Gombani Pemba kwa kukusanya wanariadha kutoka ndani na nje ya Nchi, ambapo Mgeni rasmi wa mbio hizo anatarajiwa kuwa makamo wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla “Naomba nitowe wito wangu kwa wananchi Watanzania wote wapenda maendeleo kuweza kushiriki katika mbio hizi na pia kuweza kutoa michango yao kwa ajili ya kusaidia Watu Wenye Ulemavu” amesema Aliongeza kuwa Mbio hizo zinatarajiwa kuwa mbio za Nusu Marothon zikijumuisha mbio za Kilometa...

TAMWA ZNZ yataka adhabu kali kwa wahalifu wa Udhalilishaji kwa Watoto.

Image
CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar, (TAMWA ZNZ) kinawataka wasimamizi wa watoto kuzingatia haki za watoto kwa kuhakikisha wanalindwa na adhabu kali zinatolewa kwa wahalifu wa vitendo vya udhalilishaji kwa mujibu wa sheria. Ripoti iliyotolewa na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar hivi karibuni inaonesha jumla ya matukio 165 ya ukatili wa kijinsia yaliripotiwa kwa mwezi Julai 2024, ambapo waathirika wengi walikuwa ni watoto. Ripoti inaonesha idadi ya watoto ni 142 sawa na asilimia 86.1 ya waathirika wote, ambapo wasichana walikuwa 115 sawa na asilimia 81.0 na wavulana 27 sawa na asilimia 19.0. Hali hii inasikitisha na inahitaji kudhibitiwa na wadau wote wakiwemo Serikali, taasisi za jamiidini, wazee, walimu na watoto wenyewe kupewa elimu ya kujilinda na kujikinga dhidi ya watu waovu. Wadau pia wanapaswa kuangalia upya ni kwa jinsi gani wanaweza kutatua changamoto zinazopelekea ongezeko la ukatili kwa watoto ambao ki msingi wanahitaji kulindwa kwa nguvu zot...